kuwa, huwa hana mzuka wa kudumu na mpenzi mmoja kwa muda mrefu akidai kuwa, wakizoeana
sana inakuwa kero kwake.
Akizungumza na GPL hivi karibuni, Uwoya alisema
kuwa haoni sababu ya kukaa muda mrefu na
mpenzi kwa sababu siyo baba yake wala mama yake na anapoamua kuchukua uamuzi wa
kumuacha wala haumiagi.
“Yaani mimi kukaa muda na mwanaume sipendagi kabisa na sina mzuka huo kweli. Ndiyo maana
mtu nikiamua kumbwaga anahaha na wengine watabembeleza weee lakini wala sina tabia ya
kurudi nyuma, kwa kifupi sipendi kudumu na
mpenzi,” alisema Uwoya aliyewahi kuwa kwenye
uhusiano na wanaume mbalimbali kabla ya
kuolewa na msakata kabumbu raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ambapo ndoa yao haikudumu.
Chapisha Maoni