Mwanamuziki maarufu wa Marekani Beyonce amewataka wamarekani kufikikisha hasira na mkanganyiko kwa wanasiasa na wabunge wao
kufuatia mauaji ya kibaguzi dhidi ya wamarekani weusi.
Watu maarufu nchini Marekani wamekua
wakielezea hisia zao kuhusu kisa cha hivi karibuni
ambapo polisi walionekana wakimpiga risasi
mwanaume mweusi wa kimarekani.
Beyonce amesema ''sote tuna uwezo wa
kuonyesha hasira zetu kwa vitendo'', akiwataka
waMarekani kuwasiliana na wanasiasa wao
wilayani na kudai haki ya kijamii na mabadiliko ya
kisheria.
Beyonce alitulia kimya kwa muda wa dakika moja
wakati wa onyesho lake mjini Glasglow jana usiku
kuwakumbuka wamarekani wawili waliouawa kwa
kupigwa risasi, na kuweka majina yao Alton
Sterling na Philando Castile kwenye screen kubwa
huku akitoa wito wa kumalizika kwa ''vita dhidi ya
walio wachache'' nchini Marekani
Mumewe Beyonce Jay Z ametoa wimbo mpya
kuhusu ufyatuaji risasi. Katika wimbo wake wenye
miondoko ya rap Jay Z anahoji kwanini Marekani
haibadili sheria yake kuhusu silaha?.
Jumanne picha nyingine ya video ilijitokeza
ambapo polisi wawili wa kizungu walionekana
wakimsukuma chini na kumpiga risasi Alton
Sterling mjini Louisiana.
Siku iliofuatia mkanda mwingine wa video
uliorekodiwa moja kwa moja kwenye Facebook -
ulidaiwa kuonyesha athari za kupigwa risasi na
polisi kwa Philando Castile katika gari lake
Minnesota.
Matukio haya yamezua mjadala mkubwa juu ya
ukatili wa polisi nchini Marekani.
Licha ya Jay Z wanamuziki wengine wa Marekani
kama Chris Brown, Solange Knowles na Swizz
Beatz pia wametoa nyimbo kuhusu mauaji ya
kibaguzi nchini Marekani.
Chapisha Maoni