watu kujichora tattoo sio jambo geni. Wapo
wanaojichora kwa ajili ya kuwaenzi wenza wao
kwa maana wapenzi, wao, watoto na hata familia
zao. Huchora picha ama majina na hata herufi za
wahusika mradi kuonyesha namna
wanavyowazimia na kuwajali. Kwa mfano katika
soka, nyota wa kimataifa wa Sweden,
aliyetangaza kustaafu kuichezea nchi yake, Zlatan
Ibrahimovic ana michoro 14 tofauti mwilini
mwake.
Kwa kuwa dunia ya leo ni kama kijiji, baadhi ya
mastaa wa Tanzania wameingia kwenye mkumbo
wa kujichora tattoo, nyingine za kuonyesha
mahaba yao kwa wenzao wao na nyingine kama
shukrani kwa kile walichofanyiwa na watu ama
rafiki zao za karibu.
Mwanaspoti linakuletea orodha ya mastaa ambao
waliojichora tattoo za wasanii wenzao kwa
kuashiria mahaba mazito waliyonayo kwao
pamoja na shukrani kwa mazuri waliyofanyiwa na
waliowaandika au kuyachora majina yao.
AUNTY EZEKIEL
Diva kutoka katika kiwanda cha filamu nchini,
Aunty Ezekiel a.k.a Mama Cookie aliyewahi
kuhusishwa kutoka na tajiri Jack Pemba na
Hartmann Mbilinyi kabla ya kuolewa na Sunady
Demonte, kafa kaoza kwa mwenza wake wa sasa,
Moze Iyobo.
Kimwana huyo amejichora tattoo mgongoni
mwake yenye jina la mzazi mwenzie huyo
waliyebahatika kupata naye binti aitwaye Cookie,
chini ya jina la mtoto huyo.
CHUCHU HANS
KATIKA hali inayoonesha mahaba yamemkolea
dhidi ya mwenza wake, Vincent Kigosi ‘Ray’,
mwigizaji Chuchu Hans ameamua kuugeuzi mwili
wake kama pambio kwa kuandika jina la waubani
wake.
Chuchu amejichora tattoo inayosomeka kwa jina
la Ray, huku Ray naye akijiandika jina la Chuchu
Hans. Wacha mahaba yawaue bhana!
NUH MZIWANDA
Kipindi cha mahaba niue baina yake na Shilole,
Nuh Mziwanda ilikuwa ngumu kumwambia
chochote kwa mwimbaji na mwigizaji huyo.
Alikufa na kuoza kwa Shilole, kiasi cha kufikia
hatua ya kujichora mkononi tattoo ya sura ya
Shilole na maneno ya Shishi baby, huku Shilole
naye akiliandika jina la Nuh juu ya kifua chake,
kuonyesha mahaba yake kwa king’asti wake.
Hata hivyo, wawili hao kwa sasa wamemwagana,
kila mtu sasa akila raha zake katika kiota kipya
cha mahaba na tayari Shilole ameshafuta tattoo
ya Nuh iliykuwa kifuani na Nuh ameshapata
mpenzi mpya ambaye atamfanya afute tattoo
yake.
HARMONIZE
Chipukizi huyu wa muziki wa kizazi kipya kutoka
Lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa kimataifa,
Diamond Platinumz, amechora tattoo ya picha ya
Diamond Platnumz kwenye mkono wake na
kuandika jina la Simba.
Harmonize alisema katika maisha yake hakuwahi
kuwaza kama itatokea siku akajichora tattoo,
lakini kutokana na mchango wa Diamond hana
jinsi.
Mwimbaji huyo alisema kwa jinsi alivyothaminiwa
na Diamond akiwa ametoka katika manyanyaso
na kudharaulika, anaona hana jinsi ila kujichora
mchoro huyo.
KAJALA
Mwigizaji mwingine wa filamu nchini, Kajala
Masanja naye yumo katika orodha hii baada ya
kuonyesha shukrani zake kwa shoga yake wa
zamani, Wema Sepetu. Kajala aliamua kuandika
jina la Wema mgongoni mwake, baada ya
Madame kumuokoa asiende kuozea jela kwa
kumlipa Sh. 13 milioni baada ya kukutwa na
hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na
mwenza wake ya utakatishaji wa fedha mwaka
2013.
Kajala aliwahi kusema aliamua kujichora jina la
Wema kama ishara ya kuonyesha shukrani kwa
msanii mwenzake huyo, kabla ya wawili hao
kutibuana na kuwa kama paka na chui.
DARK MASTER
Rapa memba wa Kundi la Chamber Squad,
amejichora tattoo yenye majina ya marehemu
Ngwea na Geez Mabovu.
Dark Master alikuwa mtu wa karibu na rapa hao
na amedai kuwa misiba hiyo miwili ni pigo
kubwa kwake, hivyo kujichora tattoo hizo ni
ishara ya upendo kwa wakali hao waliotangulia
mbele ya haki.
Rapa huyo ambaye alikuwa mnywaji pombe na
mvutaji sigara sana kwa sasa ameamua kuokoka
akiachana na vitu hivyo.
Mwanaspoti
Chapisha Maoni