0
Jina la Arsene Wenger liko juu kabisa katika
orodha ya chama cha soka cha England - FA-
kuziba nafasi ya Roy Hodgson aliyejuzulu umeneja
wa England baada ya kutolewa kwenye michuano
ya Euro 2016 (Daily Star), mabingwa wa Ligi Kuu
ya England Leicester City wanakaribia kumsajili
winga kutoka Ireland, Roby Brady, 24 anayechezea
Norwich (The Sun), Manchester United
wameongeza dau na kufikia pauni milioni 35
kumtaka kiungo mshambuliaji Henri Mkhitaryan,
27, kutoka Borussia Dortmund (Kicker), meneja wa
Manchester City Pep Guardiola atajaribu
kufanikisha uhamisho wa beki wa Everton John
Stones, 22 na mshambuliaji wa Celta Vigo Nolito,
29, ambao wote timu zao zimetolewa kwenye Euro
2016 (Manchester Evening News), Nolito, anasafiri
kwenda Manchester kwa ajili ya mazungumzo
huku akikaribia kukamilisha uhamisho wake
kwenda Manchester City kwa pauni milioni 13.8
(The Telegraph), mshambuliaji kutoka Argentina
Gonzalo Higuain, 28, hatoongeza mkataba wake
Napoli kwa mujibu wa wakala wake (Radio
Continental), rais wa heshima wa Inter Milan,
Massimo Morati ameitaka klabu yake kumsajili
Dimitri Payet kutoka West Ham, baada ya wamiliki
wapya wa Inter kutoka China kutoa kitita kikubwa
cha usajili (The Mirror), Southampton huenda
wakawazidi Stoke City katika kumsajili
mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22,
kwa kutoa pauni milioni 16 (The Sun), kipa wa
Newcastle, Tim Krul, 28, huenda akajiunga na
Middlesbrough, wakati Rafa Benitez akijiandaa
kukamilisha uhamisho wa kipa wa Gent, Matz Sels,
24, kwa pauni milioni 5 (Daily Star), Crystal Palace
huenda wakashindwa kumsajili mshambuliaji wa
Ubelgiji Michy Batshuayi, 22, licha ya kutoa dau la
pauni milioni 30. Klabu yake Marseille inataka
kumuuza kwa klabu inayocheza Champions League
(Croydon Advertiser), Batshuayi badala yake
atasaini kujiunga na Tottenham (Daily Mail), Crystal
Palace wako tayari kumtaka winga wa Newcastle
Andros Townsend, 24 (Chronicle), Crystal Palace
wanakaribia kukamilisha usajili wa kipa Steve
Mandanda, 31, kwa uhamisho usio na malipo
kutoka Marseille (The Guardian), meneja mpya wa
Everton Ronald Koeman anataka kumsajili winga
kutoka Poland Kamil Grosicki, 28. Mchezaji huyo
wa Rennes anaweza kupatikana kwa pauni milioni
10 (Liverpool Echo), kipa kutoka Uholanzi Maarten
Stekelenburg, 33, huenda akaungana na meneja
wake wa zamani Ronald Koeman, baada ya
kucheza kwa mkopo Southampton msimu uliopita
akitokea Fulham (De Telegraaf), matumaini ya
Sunderland kumrejesha tena kiungo Yann M’Villa,
25, aliyecheza kwa mkopo Stadium of Light msimu
uliopita yameongezeka baada ya mchezaji huyo
kufanyishwa mazoezi peke yake katika klabu yake
ya Rubin Kazan (Chronicle), Roma wanakaribia
kukamilisha usajili wa beki wa Manchester City
Pablo Zabaleta, 31 (La Gazzetta Dello Sport).

Chapisha Maoni

 
Top