uhamisho wa kiongozi wa genge linalouza
mihadarati nchini humo Joaquin "El Chapo"
Guzman hadi Marekani.
Watu wawili wamewasilisha kesi mahakamni ya
kupinga uhamisho huo.
Mawakili wa mlanguzi huyo "El Chapo" wamepinga
kuhamishwa kwake iliatumikie kifungo cha
ulanguzi nchini Marekani baada ya kutoroka jela
mara kadhaa akiwa nchini Mexico.
Mawakili wake wanadai kuwa hakuna ushahidi wa
kumhusisha na njama ya kutoroka gerezani na
wanakisia kuwa itachukuwa miaka 3 kwa kesi hizo
kuamuliwa.
"El Chapo" anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na
ulanguzi wa mihadarati nchini Marekani.
Serikali ya Mexico ilikuwa imekubaliana na
Marekani kumhamisha atumikie kifungo huko
ilimradi tu asihukumiwe kifo.
"El Chapo" alikamatwa mwezi Januari takriban
miezi 6 baada ya kutoroka gerezani akitumia njia
ya chini kwa chini.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu ni pigo kwa
serikali hizo mbili na vita dhidi ya ulanguzi wa
mihadarati.
BBC
Chapisha Maoni