0
Msanii TID ameamua kuwajulisha watu siri ya
maisha yake, hususan wale wanaomchukulia poa
kuwa amechoka, lakini si kweli.
TID
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa
Radio TID maesema tangu utotoni mwake
amelelewa kwenye familia yenye uwezo kipesa,
na kumpa urahisi wa kupata akiyoyahitaji kama
mtoto.
Akielezea historia ya wimbo wake wa zeze
ambao ndio ulimpa umaarufu mkubwa Tanzania
na Afrika Mashariki kiujumla, TID amesema yeye
ni mtoto wa mjini tena kutoka familia bora.
“Miaka ya 93, 94 kabla baba hajafariki, yeye
alikuwa ananipeleka shule town, mimi nimesoma
mjini unajua mi mtoto wa kishua, dingi alikuwa
na gari alikuwa ananipeleka shule na gari, sasa
kila siku nilikuwa nakuta mishe za watu
wanapiga zeze, nikamuuliza baba akaniambia hizi
ni nyimbo za Wagogo, sasa na mimi nikapata
idea pale kwa nini nisiiongezee kitu hii?”, alisema
TID
TID aliendelea kusema kuwa baada ya hapo ndio
akaenda kwa Majani kutaka kurekodi wimbo wa
Zeze, lakini Majani alikuwa akimzungusha kila
siku, huku akisingizia Juma Nature anarekodi
albam.
eatv.yv

Chapisha Maoni

 
Top