Michael ‘Lulu’ kudaiwa kumpora mwanaume
aliyezaa naye, chozi la mwanamitindo anayeuza
nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva,
Hamisa Hassan Mobeto linaelezwa kuwa ni laana
tosha kwa mwigizaji huyo.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mobeto,
mrembo huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye
matangazo ya nguo za kike, amekuwa akimwaga
chozi kila kukicha huku lawama zote akizielekeza
kwa Lulu.
Chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto amekuwa
akilalamika kwamba, Lulu alijua fika mwanaume
huyo ni mzazi mwenzake lakini akamchukulia na
kumsababishia maumivu ya kutelekezewa mtoto
wa kike aliyezaa na jamaa huyo mwaka jana.
“Kiukweli chozi la Hamisa (Mobeto) kila kukicha
ni laana tosha kwa Lulu. Unajua hakuna kitu
kibaya kwa mwanamke kama kuporwa
mwanaume wake waziwazi na kuachiwa
majukumu ya mtoto huku adui ukimjua.
“Kibaya zaidi ni tambo za Lulu mitandaoni.
Kitendo cha Lulu kutamba na mwanaume huyo
kinamuumiza sana Mobeto kwa sababu naye ni
mwanadamu. Ana moyo wa nyama kama Lulu
“Pia ukiacha tambo, Lulu amekuwa akisababisha
mtoto wa Mobeto anatukanwa jambo
lililomuongezea machungu kwani mtoto ni
malaika ambaye hajui chochote lakini amekuwa
akiunganishwa kwenye ugomvi huo,” kilieleza
chanzo hicho.
Alipotafutwa Mobeto hivi karibuni kuhusiana na
sakata hilo, hakuwa tayari kumzungumzia Lulu
na mwanaume huyo lakini akaweka wazi kwamba
kinachomuumiza ni mwanaye kuhusishwa na
ugomvi huo.
“Ishu ya Lulu na …(anamtaja mwanaume) siwezi
kuizungumzia, kitu ambacho kinaniumiza ni
kumwingiza mwanangu kwenye haya mambo.
Mtoto wangu anakuwa anajumlishwa katika
mambo ambayo hayamuhusu kabisa na
hakupaswa kuhusishwa,” alinukuliwa Mobeto na
kuongeza:
“Hakuna mzazi ambaye angekubali mwanaye
aongelewe kwenye mambo yasiyo mazuri.
Ningekuwa sina mtoto wala nisingeumia lakini
kwa sababu kuna mtoto ambaye hana hatia wala
hajui kinachoendelea hivyo sipendi na naumia
sana.”
Jitihada za kumpata Lulu ziligonga mwamba
baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na
hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS na
chatting za WhatsApp hakujibu.
Ishu hiyo ya laana kwa Lulu ilipigiliwa msumari
na mama wa marehemu Steven Kanumba
alipozungumza na wanahabari wetu hivi karibuni
katika futari iliyoandaliwa na mwigizaji Illuminata
Poshi ‘Dotnata’, nyumbani kwake, Ubungo jijini
Dar.
Alisema Lulu analiliwa na wanawake wengi kwani
wapo ambao alikuwa na uhusiano na waume zao
wakafariki dunia huku wengine wakiachwa na
watoto wadogo na kubaki wakilea wenyewe.
“Lulu ana machozi ya wanawake wengi, Mungu
anaona na ninaamini machozi hayo hayataenda
bure ipo siku atakuja kuvuna anachopanda kwa
sasa,” alisema mama Kanumba pasipo kutaja
wahusika moja kwa moja.
Chanzo:GPL
Chapisha Maoni