0
Msanii mkongwe wa bongo fleva, Afande Sele
ameongea na Enews na kuongelea swala la
wasanii wengi wa kitanzania ‘kufeki’ maisha yao
halisi ikiwemo kubadili hata rangi za ngozi zao
na kujiongezea weupe na wakati mwingine hata
kubadilisha asili yao.
Hata hivyo Afande Sele amesema ni kutokana na
uelewa wao kuwa mdogo kwa kuwa kubadilisha
muonekano hakuchangii kazi anayofanya msanii
kuwa bora, bali ubora wa kazi yenyewe ya sanaa
ni kutokana na ubunifu na utofauti katika kazi.
Afande sele amewataja baadhi tu ya wasanii wa
kiafrika ambao wamefanya vizuri kimataifa kama
kina MIRIAM MAKEBA, MADONA na wengine
wengi bila kujibadilisha wala kuongeza kitu
chochote katika ngozi zao au mionekano yao.
Afande amemaliza kwa kuwasihi wasanii wenzake
kupunguza kufeki maisha yao.
Eatv.tv

Chapisha Maoni

 
Top