Kuu ya England, huenda zikakumbwa na
wakati mgumu kutokana na kujitoa nchi hiyo
katika Umoja Ulaya, wameonya wataalamu.
“Ada za uhamisho na malipo kwa wachezaji,
yanaweza kuongezeka,” alisema Simon
Chadwick, Profesa wa Michezo katika Chuo
Kikuu cha Salford.
“Klabu zinaweza kusajili wachezaji kwa
gharama kubwa na sababu ni kushuka
thamani ya Pauni,” Chadwick aliiambia BBC
Sport.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka England, Greg
Dyke naye alisema uamuzi wa England
kujiondoa Umoja wa Ulaya unaweza
kusababisha mengi katika Ligi Kuu ya nchi
hiyo.
Alisema kuwa matokeo ya kujiondoa EU
hakuwezi kuonekana kwa miaka miwili lakini
matokeo hasa yataonekana baada ya muda
mrefu.
“Itakuwa aibu sana ikiwa wachezaji wakubwa
duniani watashindwa kuja hapa, lakini sidhani
kama hilo linaweza kutokea. Kama idadi
itapungua, itategemea na watakaokuja,”
alisema Dyke.
Alisema: “Wasiwasi wangu ni kuwa kutakuwa
na kuanguka kwa wachezaji wa Ligi Kuu katika
vikosi vya kwanza…tuna anguko na kuteteleka
uchumi kwa asilimia 30, hii ni aibu sana.
“Ikiwa wachezaji wa Ligi Kuu wataongezeka,
hiyo itakuwa safi. Lakini hatutaki kupoteza
kasi ya wachezaji wageni kuja.”
“Uamuzi huo kwa upande mwingine, utasaidia
kwa kiasi kikubwa kuwapa nafasi wachezaji
chipukizi kupata nafasi katika vikosi vya
kwanza katika timu mbalimbali,” alisema
Gordon Taylor, Mtendaji Mkuu wa Chama cha
Wachezaji wa Kulipwa.
“Hawa vijana mara nyingi hawapati nafasi, huu
sasa ni wakati wao. Wanakuwa na klabu tangu
wakiwa na miaka minane hadi 16 na kwa
uchache vijana 500 kati ya 600 hawachezi
wanapofikia miaka 21,” alisema Taylor.
Uchunguzi wa BBC unasisitiza kuwa matokeo
ya England kujiondoa EU kutasababisha
mambo mengi katika ligi hiyo ikiwamo ujira
wa wachezaji, kuandaa mashindano makubwa
na thamani ya jina la Ligi Kuu kupotea.
Nick Chadwick, mchezaji wa zamani wa
Manchester United alisema: “Soka yetu
iliyokuwa ikitamba kwa muda mrefu,
itaathiriwa na Umoja wa Ulaya.
“Sasa ni kutengeneza njia mpya na mawazo
mapya kuelekea kule ambako hatujafahamu
jambo la kufanya na hiyo inaweza kuwa kwa
miaka mitano hata 10.”
Alisema: “Kitu cha kwanza tutakachokiona
hapa ni hili la usajili. Tulichokiona kwa saa
chache ni kuporomoka kwa kiasi fulani usajili.
“Wachezaji watashindwa kuja England ikiwa
thamani ya mishahara yao itaanguka,”
aliongeza Chadwick.
Hata hivyo, alisema kuwa Ligi Kuu itaendelea
kuwa ligi kubwa na bora yenye mafanikio na
ushindani nyumbani na duniani bila kujali
matokeo ya kura ya uamuzi.
“Hakika, tutaendelea kushirikiana na serikali
na vyombo vingine na wadau.”
Baadhi ya wadau walisema kuwa kujindoa kwa
England kutapunguza uhuru wa wachezaji
kuhamia sehemu moja na nyingine.
Uchambuzi wa BBC mapema Machi wakati wa
vuguvugu hilo unaonyesha kuwa katika
England na Ligi Kuu ya Scotland, wachezaji
332 watakosa sifa za kuchezea timu hizo.
Klabu ya Scotland ya Hamilton Academical
italazimika kubadili sera ya kusajili, na kocha
Martin Canning alisema kuwa wachezaji
wanane wataathirika huku urahisi wa kuja
England ukiwa kwa wachezaji nje ya Umoja wa
Ulaya.
“BBC ilisema kuwa mchezaji kama N’Golo
Kante wa Leicester, ni wazi atashindwa
kuchezea timu hiyo hadi afuate utaratibu za
kibali,” alisema Chadwick
Chapisha Maoni