0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda ametangaza vita na makaka poa
(mashoga) na madada poa (makahaba)
walioko jijini Dar es Salaam kuwa
utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.
Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia
hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii
kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa
ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo
vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na
maadili ya mtanzania.
Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii
kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa
yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili
kuhakikisha anawamaliza wote mkoani
Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka
siku za hivi karibuni baada ya kituo cha
televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga
mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na
kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga
na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.







@udaku special

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top