Baada ya kuona kambi ya Uturuki haijazaa matunda mzuri, kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Yanga ya jijini Dar es
Salaam kitaondoka nchini mapema wiki ijayo kwenda Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wake wa tatu wa Kundi A dhidi ya Medeama
kutoka Ghana.
Yanga inatarajiwa kuikaribisha Medeama Julai 16 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati
mechi nyingine ya kundi hilo itakuwa ni kati ya
Mouloudia Olympique Bejaia (Mo Bejaia) dhidi yT TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Akizungumza na Nipashe jana, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa kikosi chao kinatarajia kwenda
Zanzibar mapema wiki ijayo na huenda wakacheza
mechi moja ya kirafiki wakiwa huko endapo benchl la ufundi litahitahi.
Saleh alisema kuwa kuanzia Jumatatu kikosi cha
timu hiyo kitafanya mazoezi makali kwa sababu
wanatarajia kutumia mfumo tofauti kufuatia
wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza
wanatarajia kuukosa mchezo huo unaofuata.
"Kesho (leo) tutafanya mazoezi kama kawaida,
Jumapili kutakuwa na mapumziko na wiki ijayo
mipango ikienda vizuri, tunatarajia kwenda
kujichimbia Zanzibar, tutatulia na wachezaji akili
yao itakuwa ni kujipanga kusaka ushindi," alisema
meneja huyo.
Yanga ndiyo inaburuza mkia katika Kundi A
ambalo linaongozwa na TP Mazembe yenye pointi
sita, Mo Bejaia yenye pointi nne ikifuatiwa na
Medeama iliyoambulia pointi moja.
Wawakilishi hao pekee wa Tanzania waliobakia
kwenye mashindano ya kimataifa wamepoteza
mechi mbili ya kwanza ikiwa ugenini Algeria
walipofungwa bao 1-0 na wenyeji na Jumanne
iliyopita ilipolala tena 1-0 dhidi ya TP Mazembe.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Mdachi Hans
van der Pluijm amesisitiza kuwa 'kimahesabu'
kikosi chake bado kina nafasi ya kusonga mbele
katika mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho
endapo itashinda mechi zake nne zilizosalia.
Chapisha Maoni