0
RUFANI ya Jamhuri kupinga hukumu ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro
kumwachia huru Sheikh Ponda Issa Ponda, dhidii ya kosa la kushawishi wakazi wa mkoa huo
kufanya kosa, ilikwama kuendelea jana na kuahirishwa kwa wiki tatu baada ya mawakili wa
utetezi kuomba muda wa kujadili na mteja wao.
Jana kesi hiyo ilitajwa na Jaji Edson
Mkasimongwa katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Malangwe Mchungahela alidai
kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana kwa ajili ya
kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza.
Hata hivyo, mawakili wa utetezi, Abubakar Mohammed na Juma Nassoro, kwa nyakati tofauti
waliomba mahakama kuwapa muda wa
kuzungumza na Sheikh Ponda, kama wataendelea kutoa huduma kwake ama la.
Nassoro alidai kuwa makubaliano yao ya awali ya
kumtetea katika mahakama ya chini
yalishamalizika, na hakuna maelekezo yoyote ili kuweza kumuwakilisha mahakamani hapo. Jaji
Mkasimongwa alisema kesi hiyo itasikilizwa Julai
23.
Katika rufani hiyo, upande wa Jamhuri
uliwasilisha hoja nne ikiwemo, mahakama ya chini ilikosea kwa kutokuzingatia uzito wa
ushahidi wa kielektroniki katika kutoka uamuzi wake.
Sababu ya pili na ya tatu, Jamhuri inadai,Hakimu Mary Moyo alikosea aliposema hati ya
mashtaka ilikuwa na mapungufu ya kisheria na
Sheikh Ponda hakuwa na nia ya kushawishi
umma wa mkoa huo kufanya kosa siku ya tukio.
Sababu ya mwisho ya Jamhuri katika kupinga
kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda ni kwamba
hakimu alikosea kusema kuwa ilishindwa
kuthibitisha kosa bila kuacha shaka.









chz
@Mpekuzi

Chapisha Maoni

 
Top