Klabu ya Azam FC imewatoa kwa mkopo wachezaji
wake wawili kipa Mwadini Ali na mshambuliaji
Ame Ali ‘Zungu’.
Afisa habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga
amesema, Klabu ya Simba ilituma barua kwa lengo
la kuwahitaji wacheza hao na wameshakubaliana
kwa ajili ya kuwatoa kwa msimu mmoja kuitumikia
klabu hiyo.
Jaffery amesema, wachezaji hao watajiunga na
klabu ya Simba iliyo mkoani Morogoro kwa ajili ya
kambi ya maandalizi ya Ligi kuu ya soka Tanzania
Bara.
Wiki iliyopita Simba ilileta wachezaji wawili kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kiungo
Sanga Bahende na mshambuliaji Cedrick Masanga,
wote kutoka FC Lupopo ya Lubumbashi.
Wakongo hao walifanya idadi ya wachezaji wa
kigeni waliokuja kwa majaribio Simba kufika saba,
baada ya mabeki Mzimbabwe, Method Mwanjali,
Janvier Besala Bokungu, kiungo Mussa Ndusha
wote kutoka DRC, washambuliaji Frederick Blagnon
kutoka Ivory Coast na Ndjack Anong Guy Serges
kutoka Cameroon.
Mbali na wachezaji hao wa kigeni, kuna wapya
wengine ambao ni pamoja na watatu waliosajiliwa
kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, wote viungo
Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Shizza
Kichuya na Jamal Mnyate kutoka Mwadui FC.
Wengine ni Moses Chibandu, Said Mussa, Kelvin
Falu, Vincent Costa wote wapya pamoja na wa
zamani Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Juuko
Murshid, Vincent Angban, Awadh Juma, Said
Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis
Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja
Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto,
Danny Lyanga na Ibrahim Hajib.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni