0

Mdau na shabiki mkubwa wa Simba Mo Dewji
ameweka hadharani nia yake kutaka kununua
klabu Simba, na malengo yake ameainisha
Bilionea wa Kitanzania Mohammed ‘MO’ Dewji
ambaye ni mkurugenzi wa makapuni ya
Mohammed Interprises (MeTL) leo amevunja
ukimya na kuweka bayana nia yake ya kutaka
kununua asilimia 51 za klabu hiyo kwa shilingi
bilioni 20 za Tanzania.
MO amesema Kwenye Mkutano wa Waandishi wa
Habari leo nia yake ya kutaka kuwekeza kitita
hicho cha pesa ni kutaka kufanya mabadiliko ya
mfumo mzima wa uendeshaji wa klabu hiyo ili
kuleta ushindani ndani ya nchi na kimataifa lakini
kubwa ni kuhakikisha klabu hiyo inapata
mafaniko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma
wakati akiidhamini klabu hiyo.
“Nakumbuka mwaka 2004 nilisema mfumo huu
wa uendeshaji hauko endelevu, na hatuwezi
kuendelea kushindana na klabu kubwa za Afrika
kama Ismailia, TP Mazembe na nyingine kama
tukiendelea na mfumo huu ambao tunao.
Niliwaomba sana viongozi tubadilishe mfumo
lakini kwa bahati mbaya miaka 10 iliyopita
ilionekana kama haiwezekani.”
Baada ya kusema hivyo, MO Dewji akaanza
kuorodhesha kwa nini anataka kuwekeza kwenye
klabu ya Simba ili kuleta mafanikio na ushindani
zaidi.
Moja ya mambo yaliyomsukuma kutaka
kuwekeza kiasi hicho cha pesa ni kuboresha
mishahara ya wachezaji ambao wanalipwa kiasi
kidogo ukilinganisha na timu shindani za Yanga
na Azam ambazo zimekuwa zikilipa vizuri
wachezaji wake na ndiyo maana zimekuwa
zikifanya vizuri.
Kitu kingine MO amesema ni kutaka kuipa Simba
uwezo wa kusajili mchezaji inayemtaka kama
ilivyo kwa washindani wake Yanga na Azam
ambazo zimekuwa zikimwaga kiasi kikubwa cha
pesa kwa mchezaji inayemtaka na kiweka
pembeni timu hiyo hata kama ahadi yao ni
milioni 20.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top