Anthony Martial ameitosa Manchester United
kutoka kwenye kurasa za twitter alizokuwa
akizifuata baada ya kubadilishiwa namba ya
fulana yake
Nyota huyo wa miaka 20 aliyetua Old Trafford
msimu uliopita wa majira ya joto, ameipoteza
namba yake pendwa ya fulana badala yake
amepewa jezi namba 11 kwa msimu ujao ili
kumpisha Zlatan Ibrahimovic.
Martial alizua tetesi za kutokuwa na furaha kwa
mabadiliko hayo Jumamosi kwa kutupia picha
kwenye ukurasa wake wa Facebook ikimwonesha
akiwa ndani ya jezi ya namba tisa baada ya
kufunga goli katika mechi ya nusu fainali Kombe
la FA dhidi ya Everton.
Sasa Mfaransa huyo ameamua kwenda mbali
zaidi kwa kuiondoa klabu hiyo kwenye ukurasa
wake wa Twitter na Instagram Jumapili asubuhi.
Martial si sehemu ya kikosi cha United kilichopo
ziarani China kwani anaendelea kufurahia likizo
yake baada ya fainali za Euro 2016 zilizofanyika
Ufaransa.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni