Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameweka
mkazo kwamba yupo tayari kutumia pesa kusajili
mchezaji sahihi ambaye ni anaweza kufiti kwenye
mfumo wake.
Mpaka sasa, Arsenal wamefanikiwa kutumia kitita
kikubwa kumsajili Granit Xhaka na baadaye
kuwachukua Mjapani Takumo Asano na Rob
Holding
Wenger amekuwa akikosolewa kwa kushindwa
kwake kusajili wachezaji wenye majina makubwa
hasa kwenye nafasi ya beki wa kati na
ushambuliaji licha ya wapinzani wake wengi
kufanya hivyo.
Hata hivyo Wenger amesema kwamba bado
hajamaliza kusajili ila anaangalia mtu sahihi wa
kumleta kwenye timu yake.
“Tuna mwamko mkubwa. Kama tunapata mchezaji
sahihi basi hatuwezi kusita kutumia pesa
kumsajili,” Wenger aliimbia tovuti ya klabu baada
ya sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kirafiki
dhidi ya Lens.
“Mpaka sasa tayari tumetumia pesa nyingi. Kwa
ujumla tayari tumeimarisha kikosi chetu kwa kiasi
kikubwa lakini hata hivyo bado yuko macho
kwenye dirisha la usajili.
“Nisingeoenda kuangalia zaidi majina, kwasababu
kama hujawapata, watu watakuuliza kwanini. Tuko
makini, tena makini sana kila siku na hatujamaliza
zoezi la usajili. Ndiyo kwanza tarehe 22 leo (jana)
na dirisha la usajili linafungwa Agosti 31. Na
unafahamu fika kwamba mambo mengi hutokea
wiki ya mwisho. Hivyo bado kuna safari ndefu.
Lakini tupo makini na tunalifanyia kazi suala hilo.
Mpaka leo hakuna aliyetumiapesa nyingi kutuzidi
katika usajili nchini hapa. Hata kama [Paul] Pogba
anataraji kuja hapa kutokea Italy, sijui…
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni