0
Waziri Mkuuwa Israel benjamin Netanyahu
anakamilisha ziara yake barani Afrika Alhamisi
nchini Ethiopia ambapo anatarajiwa kukutana na
viongozi wa serikali na kutia saini mikataba
kadhaa ya maendeleo. Tangu kuwasili kwake
barani Afrika Julai 4, Netanyahu amezuru Uganda,
Kenya na Rwanda katika kile alichokitaja kama
histori kubwa kwa Israel kurejea barani Afrika.
Amekuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Israel kuzuru
Afrika katika kipindi cha miaka thelathini.
Ethiopia ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza
barani Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia
na Israel katika miaka ya sitini. Lakini uhusiano
huo umeyumba yumba mara kadhaa baada ya
Ethiopia kuukatiza mara kadhaa katika historia
yake.
Hii ilidhihirishwa zaidi wakati wa vita vya Waarabu
na Israel mwaka 1973 wakati Ethiopia iliposimama
pamoja na mataifa mengine ishirini ya Afrika;
kukatiza uhusiano kidiplomasia na Israel. Hata
hivyo maaptanao yaliafikiwa tena katika miaka ya
1980 baada ya Israel na Misri saini mkataba wa
amani mwaka 1979.
Hata hivyo, katika mwaka 1984 Ethiopia ilipokuwa
ikikabiliwa na kiangazi na migogoro ya kisiasa
wakati wa utawala wa Mengistu Haile Mariam,
Israel ilihofia usalama wa maelfu ya Wayahudi wa
Ethiopia na kuwaondoa elfu saba kati yao katika
safari za siri za ndege katika kile kilijulikana kama
kama Operation Moses. Shuguli hiyo iliisababishia
Ethiopia aibu kubwa huku awali ikidai kwamba
walikuwa wametekwa nyara. Miaka sita baadaye,
wengine elfu kumi na nne zaidi walisafirishwa hadi
Israeli katika siku mbili tu. Sasa kuna zaidi ya
Wayahudi mia moja na thelathini elfu kutoka
Ethiopia wanaoishi nchini Israeli.
Hatima ya wengine elfu tisa ambao bado wako
Ethiopia inatarajiwa kuangaziwa katika
mazungumzo kati ya serikali hizo mbili baadaye
Alhamisi. Licha ya hayo, nchi hizo mbili
zinajivunia kuwa washirika wa karibu katika vita
vya kimataifa dhidi ya ugaidi na kuwa na msaada
wa Marekani. Ziara pia anatarajiwa kuendeleza
mahusiano baina ya nchi hasa katika maeneo ya
biashara, usalama, kilimo na elimu.

BBC

Chapisha Maoni

 
Top