amejitetea dhidi ya uamuzi alioufanya wa kuiingiza
Uingereza katika vita ya Iraq mnamo mwaka 2003
kwa kushirikiana na mshirika wake Marekani baada
ya ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusu vita hivyo.
Bwana Blair amesisitiza kwamba hakuipotosha
Uingereza kuingia katika vita hivyo, ingawa
ameomba radhi kwa familia zilizifiwa na ndugu zao
wakati wa vita hivyo.
Tonya Blair amesema anaamini kwamba ulikuwa ni
uamuzi sahii wa kumuondoa kiondongozi wa
zamani wa Iraq marehemu Saddam Hussein, na
kwamba angeweza kuchukua uamuzi kama huo
wakati huu.
"Wacha tuwe wazi kuhusu uamuzi. Inatokana na
kilichotekea huko Mashariki ya kati. Na ninaamini
kwamba Iraq ingepata utulivu na Mashariki ya Kati
pia ingepata utulivu. Kuhusu tathimini yangu kwa
yale yanayoendelea huko mashariki ya kati ni
mapambano makubwa, kuondoa siasa za kidini na
kuweka siasa zinazojumuisha watu
wote,kuvumiliana, na kuvuliana dini za watu
wengine. Na uamuzi huo ilikuwa na nia ya utawala
unajenga uchumi sio uchumi wa ufisadi. Kwa sasa
nafikiri hivyo ni vitu viwili, watu wanapambana
eneo zima la Mashariki ya kati. Na Iraq chini ya
Saddam haina nafasi." alisema
viongozi waandamizi katika maamuzi nchini
Uingereza wameanza kurusha lawama kwa
mshirika wao Marekani juu ya uamuzi
uliochukuliwa mwaka 2003 dhidi ya vita vya Iraq
kutokana na athari za uamuzi huo kuzidi
kuonekana miaka kumi na nne baadaye.
Mapema wiki hii, Uingereza uchunguzi uliofanywa
na John Chilcot umeegemea kuelekeza
mashambulizi makubwa juu ya
maandalizi,utekelezaji na matokeo ya vita vya Iraq.
Jenerali Tim Cross, mmoja kati ya viongozi
waandamizi wa jeshi nchini Uingereza kushiriki
katika mipango vita hivyo,Alisema Marekani
inapambua jeshi la Iraq na chama cha Ba'ath
zilivyoingia vitani bila kufuata ushauri.
Naye Jeremy Greenstock,balozi wa Uingereza
Balozi katika Umoja wa Mataifa alinukuliwa
akisema kwamba Marekani iliisukuma jeshi la
Uingereza mapema mno, na kuongeza kusema
kwamba wachunguzi wa umoja wa mataifa
wanapaswa kutumia muda zaidi kuchunguza
masuala ya kemikali na silaha za kibaiolojia
zilizotumika katika vita vya Iraq .
Alistair Campbell,alikuwa mkuu wa kitengo cha
mawasiliano wakati wa utawala wa waziri mkuu wa
zamani wa Uingereza Tony Blair, amesema
kwamba Wamarekani hawatekelezi makubaliano
yaliyofikiwa kabla kama walivyotarajiwa
BBC.
Chapisha Maoni