Wajumbe katika kongamano kuu la chama cha
Republican nchini Marekani wamemzomea seneta
wa Texas, Ted Cruz, baada yake kukosa
kumuidhinisha Donald Trump kuwa mgombea wa
chama hicho.
Bw Cruz alikuwa amesalia kuwa mpinzani pekee
wa Bw Trump lakini akajiondoa baada ya
kushindwa katika uchaguzi wa mchujo jimbo la
Indiana mapema mwezi Mei.
Bw Cruz, akihutubu katika kongamano hilo
linalotumiwa kuamua mgombea wa chama hicho
kwenye uchaguzi mkuu Novemba, amesema tu
kwamba anataka maadili ya chama cha Republican
yashindwe kwenye uchaguzi huo.
Waandishi wa habari wanasema hatua ya Bw Cruz
kukataa kumuunga mkono wazi bw Trump
inatokana na migawanyiko ambayo imeendelea
katika chama hicho kuhusu ugombea wa Bw
Trump.
Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro
Marekani
Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle
Obama
Gavana wa Indiana Mike Pence alikubali rasmi
kuwa mgombea mwenza wa Bw Trump kwenye
kongamano hilo.
Ameeleza maadili yake ya kihafidhina na
akashambulia maadili na historia na sifa za Hillary
Clinton, mgombea wa chama cha Democratic.
Baada yake kumshutumu Bi Clinton, wajumbe
wamerudia kuimba "Lock Her Up" (Afungwe) kwa
siku ya tatu mfululizo.
Bw Trump anatarajiwa kuhutubia kongamano hilo
Jumatano.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni