baada ya chama hicho kufungua kesi mahakamani, kupinga wanachama na wapenzi wake kuwekwa
kizuizini.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu Zanzibar na inasubiri kupangiwa Jaji kabla ya kuanza
kusikilizwa kwa hati ya dharura.
Wakati CUF ikichukua uamuzi huo, polisi imetupa dai la chama hicho la juzi la kutaka wafuasi hao wafikishwe mahakamani kwa kusema haifanyi kazi
kwa matakwa ya mtu au kikundi cha watu.
Mwanasheria wa CUF, ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, Is-haq Sharif amefungua kesi kwa hati ya dharura dhidi ya Mwansheria Mkuu wa
Zanzibar na Jeshi la Polisi.
Sharif anawawakilisha aliyekuwa Mwakilishi wa
Jimbo la Kiwani, Hija Hassan Hija na Mbunge wa
Mkoani, Seif Khamis Mohamed, waliokamatwa na kuwekwa kizuizini bila kufungulkiwa mashitaka.
Wengine wanaoshikiliwa na Polisi kwa muda mrefu ni Abdultif-Saleh Khamis na Faki Suleiman
Mohamed, ambao walikamatwa Juni 29, mwaka huu, lakini hawajafikishwa mahakamni na kunyimwa haki ya kisheria ya kukutana na
mawakili. Sharif alidai kuwa kitendo cha wateja wake kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka mahakamni ni kinyume cha misingi ya haki za
binadamu na utawala wa sheria visiwani humo.
Alidai kuwa amekuwa akinyimwa haki ya kukutana na wateja wake na kusababisha kushindwa kufahamu wamefanya makosa gani na kwa nini
hawafikishwi mahakamani ndani ya saa 24 tangu kukamatwa kwao kama sheria zinavyotaka.
“Tunataka Mahakama iwaite polisi waeleze kwa nini wamewakamata wateja wangu na kuwaweka kizuizini bila kuwafungulia mashtaka,” alidai.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Zanzibar limesema linaendelea na taratibu za uchunguzi kwa watuhumiwa waliokamatwa kisiwani Pemba,
wakiwemo wanachama na viongozi wa CUF ili
kuwafikisha mahakamani.
Kauli ya jeshi hilo imetolewa baada ya CUF kulitaka
jeshi hilo kuwapaleka mahakamani, kama wana
ushahidi wa kutosha kuliko kuwaweka rumande na
kuwadhalilisha.
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar,
Salum Msangi alisema jeshi hilo linafanya kazi
zake kwa utaratibu maalum na si kushurutishwa
na mtu yoyote.
Alisema tayari watuhumiwa 50 wameshafikishwa
mahakamani na wachache waliobaki wanaendelea
kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika nao
watafikishwa mahakamani.
“Watuhumiwa wachache waliobaki ambao upelelezi
haujakamilika ni pamoja na Hija na amekamatwa
kwa kosa kubwa kuliko wengine,” alisema.
Kwa hisani ya gazeti la Nipashe, imeandikwa na
Mwinyi Sadala na Rahma Suleiman, Zanzibar
Chapisha Maoni