0
Klabu 16 za Ligi Kuu Bara zitapokea mgawo wa udhamini wa haki za televisheni wiki ijayo, imeelezwa Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Hamad Yahaya alisema mchakato wa kupata fedha kutoka kwa wadhamini Kampuni ya Azam Media uko hatua za
mwisho.
Yahaya alisema licha ya fedha hizo kuwa ndogo, lakini anaamini zitasogeza na kuzipa baadhi ya 'mapengo' kwa timu hizo.
"Kwa awamu ya kwanza, kila klabu itapata Sh. milioni 42, sisi bodi ya ligi kila tunachopokea
tunakihamisha haraka kwa klabu husika ili zisaidie mahitaji yao," alisema mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa bado bodi ya ligi haijapokea fedha
kutoka kwa mdhamini mmoja wa Ligi Daraja la
Kwanza na mara watakapopokea, watazilipa timu
zote Sh. milioni 8 wanazodai.
Kuhusiana na zawadi za msimu uliopita, kila
anayestahili kupata, atalipwa katika sherehe
maalumu iliyoandaliwa na wadhamini wakuu
Vodacom itakayofanyika Julai 17.

Chapisha Maoni

 
Top