sita jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake mwaka 2013 lakini alikata rufaa
iliyopelekea uamuzi wa mahakama dhidi yake
kisheria kuchukua takriban miaka mitatu.
Katika tukio la aina yake mwezi uliopita wakati wa
kusikilizwa kwa shauri hilo kuhusu adhabu
aliyopewa mwanariadha huyo alishauriwa na timu
ya wanasheria wanaomtetea kuvua miguu ya
bandia na kutembea kwenye chumba cha
mahakama bila miguu hiyo.
Ili kutoa ushawishi kwa jaji kuamini kuwa hakuwa
na uwezo wa kufanya mauaji hayo.
Pistorius tayari ameshatumikia kifungo cha
takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati
alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia
mwaka 2013.
Kwa sasa kifungo chake kimeongezeka baada ya
upande wa serikali kushinda rufaa hiyo ambapo
kosa lake lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa
kukusudia.
Hata hivyo hukumu hiyo imepingwa vikali na
makundi mbalimbali ya watu nchini Afrika Kusini
wakidhani alistahili kufungwa miaka mingi zaidi
kutokana na kosa alilofanya.
Chapisha Maoni