Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya
Uingereza Demba Ba amesema hataacha kucheza
soka hata baada ya kuvunjika mguu akicheza.
Ba, ambaye kwa sasa huchezea Shanghai
Shenhua, alivunjika mguu baada ya kukabwa
akicheza mechi ya Ligi Kuu ya Uchina.
Baada ya mechi hiyo, mkufunzi wa mshambuliaji
huyo wa Senegal Gregorio Manzano alisema jeraha
hilo “huenda likafikisha kikomo uchezaji wake”.
"Hili ni jeraha mbaya sana lakini ninaweza
kujikwamua. Sitafikisha kikomo uchezaji wangu
hapa, hilo nina uhakika nalo,” amesema Ba,
mwenye umri wa miaka 31.
“Msimu hapa unamalizika Novemba na kuanza
Machi. Nitajizatiti kurejea kwa wakati kwa msimu
utakaofuata.”
Demba Ba avunjika mguu uwanjani
Demba Ba alichezea West Ham, Newcastle na
Chelsea katika Ligi ya Premia.
Alijiunga na Shenhua kutoka klabu ya Besiktas ya
Uturuki, akinunuliwa takriban pauni 12 milioni
mwezi Julai mwaka jana.
Kwa sasa, ndiye mfungaji mabao bora Ligi Kuu ya
Uchina akiwa na magoli 14 kutoka mechi 18.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni