0
Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz
kutoka Tanzania ametajwa kuwa msanii pekee
kutoka upande wa Afrika Mashariki kupanda
kwenye stage ya tamasha la Afrika litalofanyika
New York July 22.
Ni tamasha ambalo kwa mara ya kwanza
litafanyika kwenye ukumbi wa Barclays Centre,
ukumbi ambao Wamarekani wamezoea kuona
mastaa wakubwa wakitumbuiza hapo kama Jay Z.
Ni ukumbi ambao unaweza kuchukua watu mpaka
elfu 20 ambapo Diamond ameonekana
mwanamashariki pekee huku wengine wakiwa ni
Wanigeria kama Davido, Wizkid na Iyanya.

Chapisha Maoni

 
Top