0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
amewataarifu wakurugenzi wa Halmashauri za
Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya walioteuliwa tarehe
07 Julai, 2016 kuwa watakapofika Ikulu Dar es
salaam kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu uadilifu
wa uongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12
Julai, 2016 wakiwa na nakala zao halisi za vyeti
vya kitaaluma (Original Academic Certificates).
Aidha, Balozi kijazi amesema kuwa uhakiki wa
vyeti halisi vya kitaaluma (Original Academic
Certificates) unafanywa kwa lengo la kujiridhisha
baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki
kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi
(Photocopies).
Uhakiki huo wa vyeti utaanza saa mbili asubuhi na
wahusika wote wameombwa kuingia Ikulu kwa
kupitia geti kuu la lililopo upande wa mashariki.

Chapisha Maoni

 
Top