wanawake duniani Serena Williams amemshinda
mchezaji nambari nne duniani kutoka Ujerumani
Angelique Kerber ili kushinda taji la saba la
Wimbledon na taji 22 la Grand Slam.
Raia huyo wa Marekani alikabiliana na upepo mkali
kushinda seti 7-5 na 6-3 na hivyo basi
kusawazisha rekodi iliokuwa ikishikiliwa na Steffi
Graf ya kushinda mataji muhimu.
Kerber alimshinda Williams katika mashindano ya
Australia Open mnamo mwezi Januari,lakini
hakuweza kumshangaza tena katika taji la Grand
Slam.
William sasa amemaliza msururu mbaya wa
kushindwa katika Grand Slam ulioanza katika taji
la Wimbledon mwaka uliopita.
BBC
Chapisha Maoni