Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira
amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini Frank Charles Msaki kutokana na
makosa ya kufanya malipo hewa ya kulipa posho
ya chakula kwa watu ambao si askari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara,
Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki
anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi
cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa
watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia
mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa
Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi anayetakiwa
kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’
ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote
yule.
Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha
kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai,
2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma
zinazomkabili.
Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la
uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu
kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi
imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili
kufanikisha malipo hayo hewa.
Chapisha Maoni