KIUNGO wa kimataifa wa
Ufaransa, Paul Pogba
atakuwa mchezaji wa
Manchester United tena
baada ya kufikia makubaliano
ya dili la uhamisho wa Pauni
Milioni 100 na Juventus
usiku wa Alhamisi.
Inamaanisha mchezaji huyo
aliyeondoka Old Trafford bure
mwaka 2012 atarejea kama
mchezaji babu kubwa -
aliyesajiliwa kwa dau la
rekodi duniani.
Dili la nyota huyo wa
Ufaransa mwenye umri wa
miaka 23 linatarajiwa
kukamilishwa Ijumaa baada
ya wakala wa Pogba, Mino
Raiola kuwa na mazungumzo
ya kina na viongozi wa
Juventus na wanasheria
mjini Turin mchana wa
Alhamisi.
United na Juventus
zzimekubaliana kumlipa
Raiola sehemu ya asilimia
yake 20 katika mauziano ya
Pogba.
Pogba anatarajiwa kufanyiwa
vipimo mjini Los Angeles,
Marekani alitangulia kwa
mapumziko mjini Florida.
Na amekubali kusaini
mkataba wa miaka mitano,
ambao utamfanya alipwe
mshahara wa Puni 290,000
kwa wiki.
Pogba aliondoka Old Trafford
Julai mwaka 2012 baada ya
kocha wa Man United wakati
huo, Sir Alex Ferguson
kukataa ombi la Raiola
kuuboresha kidogo mkataba.
Juventus ililipa Pauni
800,000 kumpata.
Atakuwa mchezaji wa nne
kusajiliwa na kocha mpya,
Mreno Jose Mourinho baada
ya beki Eric Bailly,
mshambuliaji Zlatan
Ibrahimovic na kiungo
mshambuliaji Henrikh
Mkhitaryan.
Muargentina Angel Di Maria
alikuwa mchezaji ghali wa
mwisho kusajiliwa England,
akinunuliwa kwa Pauni
Milioni 59.7 na Man United
kutoka Real Madrid Agosti
mwakaa 2014.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni