Msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘ Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es
Salaam, Tanzania imetua salama jijini
Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku
10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini
kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21,
mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko
Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam na kwamba mshindi atakuwa amejiwekea
mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana,
zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi
ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la
Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo
ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime maarufu
zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, Daktari wa timu
hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa,
Andrew Vanance Andrew.
Pia yumo Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda
amechukua nafasi ya makocha wasaidizi,
Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed
‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi
ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani
Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na
Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako
Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage,
Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally
Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi
Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor
Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi
Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed
Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na
Muhsin Malima Makame.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika
Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya
mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa.
Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika
Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia
na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India
ambako walishiriki mashindano ya vijana ya
Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF
International Youth Tournament 2016) kabla ya
kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika
Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika
nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na
Marekani.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni