JUZI Jumatatu Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi,
Hans van Der Pluijm aliukabidhi uongozi wa timu
hiyo ripoti yake ya mechi ya Kombe la Shirikisho
Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana iliyofanyika
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Ripoti hiyo imedaiwa kuushtua uongozi wa timu
hiyo kutokana na mambo mbalimbali ambayo
kocha huyo ameyaainisha ndani yake
yanayohusiana na mechi hiyo ambayo Yanga
ilitoka sare ya bao 1-1. Moja ya mambo makubwa yaliyoushitua uongozi
wa timu hiyo ni jinsi kocha huyo alivyosema kuwa
wachezaji wake waliachana na maagizo yake na
kuamua kucheza wanavyojua wao. “Ukiacha hilo, ameainisha pia na mambo mengine
ambayo kimsingi siyo vizuri kuyasema lakini kwa
namna moja ama nyingine uongozi utakuwa
umeyaona na utayafanyia kazi. Kwa kifupi siyo
ripoti nzuri,” kilisema chanzo hicho cha habari. Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo Katibu Mkuu
wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema: “Ni kweli
ripoti hiyo tumeshaipokea na kocha ameainisha
mambo mengi lakini siyo vizuri kuyaweka wazi, la
msingi ninaloweza kusema ni kwamba tutaifanyia
kazi ipasavyo.
“Lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika
mechi zilizobaki hivyo tunamshukuru kocha kwa
ripoti yake hiyo na sisi kama uongozi tutayafanyia
kazi yote yanayotuhusu.”
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni