Kiungo wa Simba Jonas Mkude aliyekuwa nchini
Afrika Kusini kufanya majaribio klabu za Bidvest
Wits na Mpumalanga Black Aces amerejea nchini.
Ingawa hakuwa tayari kuweka wazi kwa sasa
kuhusiana na matokeo ya majaribio hayo
yaliyochukua takriban wiki tatu, alisema kila kitu
kilikuwa sawa na kwamba sasa anajiandaa
kujiunga na kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mkude kufanya
kazi na bosi mpya wa benchi la ufundi la timu
hiyo, Mcameroon, Joseph Omog kwani awali
wakati kocha huyo anaanza kazi kikosini hapo,
ndiyo wakati ambao Mkude alitokomea Afrika
Kusini.
“Nimerudi juzi na kila kitu kilikuwa sawa na sasa
nimerejea, nipo Dar lakini kesho (leo) nitaondoka
kuelekea Morogoro kujiunga na timu kwa ajili ya
mazoezi. Kwa sasa siwezi kuzungumzia masuala
ya matokeo, hayo nitaongelea baadaye,” alisema
Mkude.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni