0

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
amesema amaimani kikosi chake cha msimu
ujao ambacho kinaundwa na wachezaji wengi
chipukizi
Julio ameiambia Goal , ari waliyokuwa nayo
wachezaji hao unamfanya atamani kuanza kwa
ligi ya Vodacom hata leo kwani anauhakika wa
kutimiza kile ambacho amewaahidi mashabiki na
uongozi wa timu hiyo ambacho ni ubingwa.
“Ushindani umekuwa mkubwa kuanzia mazoezi
hili ni jambo zuri kwa timu yoyote ningependa
kuona ari hii waliyokuwa nayo inahamia kwenye
mechi za mashindano na kutimiza kile
nilichoahidi kwa mashabiki na uongozi wangu
ambacho ni ubingwa,” amesema Julio.
Kocha huyo mwenye maneno mengi amelazimika
kuwatema wachezaji wengi kwenye kikosi chake
cha msimu uliopita wakiwemo wakongwe
Athumani Iddi ‘Chuji’, Jerry Tegete, Nizar na
Razak Khalfan,Jabir Aziz, David Luhende, Anthony
Matogolo na Jamali Mnyate.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top