0

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa dharura,
jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa
Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na
masuala mengine, itapokea taarifa na kujadili hali
ya siasa nchini.
Katika siku za hivi karibuni, taifa limekuwa
likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa ni pamoja
na uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za
kuongoza nchi unaofanywa waziwazi na mamlaka
za juu/viongozi waandamizi wa nchi kupitia kauli
na matendo mbalimbali kiasi cha kuwashtua
Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao
ikiendeshwa katika misingi ya uwajibikaji wa
kisheria na demokrasia.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24,
mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na
kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu
mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga
chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa
ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha
misingi kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima,
kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.
Imetolewa Ijumaa, Julai 22, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top