Kikosi cha Yanga kimeondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano
wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Medeama.
Yanga watashuka uwanjani Julai 26 siku ya Jumanne kucheza mechi yao ya pili ugenini baada ya kucheza mechi mbili pia nyumbani.
Mchezo kati ya Medeama dhidi ya Yanga utachezwa kwenye uwanja wa Essipong Sports
uliopo kwenye mji wa Sekondi, Ghana. Mechi hiyo itasimamiwa na mwamuzi wa kati Redouane Jiyed
atakayesaidiwa na Mohamed Lahmidi (line one) na
Hicham Ait Abboou (line two).
Yanga itaingia uwanjani kupambana na Medeama
ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare kwenye
mchezo wa awali ilitoka sare ya kufungana goli
1-1 na kujiweka kwenye mazingira ya kusonga
mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni