0

Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona wapo nchini
Uingereza kwa ajili ya maandalizi yake ya msimu
mpya.
Kikosi hicho chini ya Luis Enrique, kinaongozwa
na nyota wake kama Lionel Messi na Luis Suarez
wakati kinawakosa Neymar na baadhi ya nyota
walioshiriki fainali za michuano ya Euro 2016
iliyofanyika nchini Ufaransa.
Neymar na Rafinha bado wako kwao Brazil
wakijiandaa kushiriki Michezo ya Olimpiki.
Kambi hiyo ya siku sita iliyo katika enero la St
George's Park, Burton-upon-Trent pia ni sehemu
ya kujiandaa na mechi dhidi ya Celtic, mechi
itakayopigwa mjini Dublin.
Messi ambaye alikatiza likizo yake na kujumuika
kwenye safari hiyo, amekuwa kivutio baada ya
kubadili muonekano wake kwa kiasi kikubwa.
Messi amebadili rangi ya nywele zake huku pia
akiendelea kufuga midevu, utaratibu uliouanza
mwishoni mwa msimu uliopita.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top