0

Manchester City, wakicheza mechi yao ya kwanza
ya kujiandaa kwa msimu mpya chini ya meneja
mpya Pep Guardiola, wamechapwa bao moja kwa
bila na klabu ya zamani ya meneja huyo Bayern
Munich.
City walifungwa bao moja na Erdal Ozturk wa
Bayern, ambao kwa sasa mkufunzi wao ni Carlo
Ancelotti.
Wachezaji wengi nyota hawakucheza mechi hiyo
kwani bado wanapumzika baada ya kushiriki Euro
2016 na Copa America.
Guardiola alichezesha wachezaji 12 wa timu ya
vijana, mechi hiyo iliyochezewa Allianz Arena.
Mlinda lango wao alikuwa Angus Gunn, mwanawe
mchezaji nyota wa zamani wa Norwich Bryan.
City sasa wataelekea Uchina ambapo watacheza
dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu.
Watasafiri na Sergio Aguero, David Silva, Nolito,
Raheem Sterling na Joe Hart.
Kikosi cha Manchester City kipindi cha kwanza:
Caballero, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino,
Fernando, Fernandinho, Zinchenko, Barker,
Iheanacho, Navas
Kipindi cha pili:
Gunn, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino,
Clichy, Fernando, Fernandinho, Delph, Bony, Navas



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top