Meneja wa sasa wa klabu ya Sunderland Sam
Allardyce anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja
mpya wa Timu ya Taifa ya England .
Bodi ya Chama cha Soka England, kitakaa
kumpitisha kama Meneja wao mpya kuchukua
nafasi ya Roy Hodgson aliemaliza Mkataba wake
Majuzi tu baada ya kwisha Fainali za EURO 2016
na England kutolewa kwenye Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 na ‘vibonde’ Iceland.
Kwenye mchakato wa uteuzi wa wadhifa huu,
Allardyce, maarufu kama Big Sam, alichuana vikali
na Meneja wa Hull City Steve Bruce aliewahi
kuichezea Manchester United.
Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn, alithibitisha
kuwa Bodi ya Watu 12 ya FA itajulishwa rasmi
kuhusu mchakato wa uteuzi wa Meneja wa Timu
ya Taifa ili itoe uamuzi kwenye Kikao chao cha
Alhamisi.
Waliopewa mamlaka ya kupendekeza nani atakuwa
Mrithi wa Roy Hodgson ni Glenn mwenyewe,
Makamu Mwenyekiti wa FA, David Gill, aliewahi
kuwa Mtendaji Mkuu wa Man United, na
Mkurugenzi wa Ufundi, Dan Ashworth.
Aliewahi kuwa Meneja wa Man United Sir Alex
Fergusonaliwaeleza wazi viongozi wa Fa kuwa Mtu
pekee anayefaa wadhifa wa Meneja wa England
kwa sasa ni Sam Allardyce – BIG SAM.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni