Chama cha Soka cha Ureno-FPF kimetangaza
kumuongeza mkataba kocha Fernando Santos
mpaka 2020 baada ya kukiongoza kikosi cha timu
ya taifa ya nchi hiyo kutwaa taji la michuano ya
Ulaya mwaka huu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye
amekuwa akikinoa kikosi hicho toka Septemba
mwaka 2014, aliiongoza Ureno kutwaa taji lake la
kwanza kubwa la kimataifa pamoja na kucheza bila
nyota wake Cristiano Ronaldo katika fainali dhidi ya
wenyeji Ufaransa mapema mwezi huu.
Mkataba wake mpya alioongezwa utamfanya
kukiongoza kikosi hicho katika michuano ya
Kombe la Dunia mwaka 2018 na ile ya ijayo ya
Ulaya. Santos amewahi kufundisha klabu kubwa
nchini Ureno zikiwemo Benfica, Sporting Lisbon na
Porto huku pia akiwahi kuinoa timu ya taifa ya
Ugiriki.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni