
Ryan Giggs amefikisha kikomo cha muda wake wa
kuhudumu katika klabu ya Manchester United
baada ya kukubali kuondoka kupitia makubaliano.
United inatarajiwa kutoa taarifa rasmi katika siku
chache zijazo kuhusu hatua hiyo.
Giggs mwenye umri wa miaka 42,alikuwa amesalia
na mwaka mmoja katika

kandarasi yake kama
Naibu Meneja, lakini mkufunzi Jose Mourinho
anataka nafasi yake ichukuliwe na rafikiye Rui
Faria.
Huku akishindwa kuafikia makubaliano ya
kuchukua wadhfa mwengine katika klabu hiyo ya
ligi kuu ya Uingereza,Giggs ambaye aliichezea
Man United takriban mara 963 amekubali
kuondoka.
posted from Bloggeroid
Chapisha Maoni