Kulingana na BBC, Kampuni moja ya mawakili yenye makao yake mjini London, inasema imeandika barua kwa serikali ya Uingereza ikitakahakikisho kuwa haitaanzisha mchakato wa
kuondoka kwenye muungano wa ulaya bila ya
idhini ya bunge.
Kampuni hiyo inasema kuwa bila ya idhini hiyo,
serikali itakuwa imefanya kinyume cha sheria na
hatua hiyo itakabiliwa kisheria.
Mawakili hao wanawakilisha kundi dogo la
wafanyibiashara na wasomi ambao hawakutajwa.
Hatua hiyo inatajwa kuwapa wabunge wanaopinga
kuondoka kwa Uingereza fursa ya kazuia mchakato
huo.
Chapisha Maoni