
(Tanesco) kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika nchi nzima pamoja na kupima utendaji
kazi wa mameneja wa shirika hilo wa ngazi ya wilaya, mkoa na kanda.
Aliyasema hayo jana baada ya kufanya
mazungumzo na Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco
pamoja na Menejimenti ya Tanesco katika kikao
kilichofanyika jijini Dar es Salaam katika ofisi za
Tanesco ikiwa ni mara ya kwanza kwa Profesa
Muhongo kufanya kikao na Bodi hiyo tangu
ilipozinduliwa Mei mwaka huu.
Muhongo ametaka ifikapo Agosti 30 mwaka huu
vitu vyote vya zamani vya shirika hilo viwe
vimekamilika na kuanza na mambo mapya, ikiwa
ni pamoja na mikataba mbalimbali na kutoa
vipaumbele vya kazi ili nchi iwe na umeme wa
uhakika utakaotosheleza mahitaji ya wananchi.
Kuhusu majadiliano ya mikataba mbalimbali,
Profesa Muhongo aliitaka Bodi hiyo kuhakikisha
kuwa majadiliano hayo yanapangiwa muda
maalumu wa kumalizika bila kuchukua muda
mrefu.
“Ifike mahala kampuni au mtu aambiwe kama
mkataba husika unawezekana au hauwezekani
badala ya kuwa na majadiliano ya muda mrefu
yasiyokuwa na ukomo, hivyo mikataba ambayo
haijakamilika, Menejimenti iiwasilishe kwa Bodi.
Tunataka ifikapo Agosti 30, 2016 vitu vyote vya
zamani viwe vimekamilika ili tuanze masuala
mapya,” alisema Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo aliitaka Bodi hiyo kuhakikisha
kuwa kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa
uhakika kwa kusimamia utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya umeme ikiwemo ya upanuzi wa
mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I, kiasi
cha megawati 185 na ujenzi wa mradi wa Kinyerezi
II wa megawati 240.
Ameitaka Bodi hiyo kujituma na kukutana kila
baada ya miezi mitatu ili kutathmini mapato ya
shirika ikiwa ni pamoja na kupima utendaji kazi wa
mameneja wa Tanesco katika ngazi ya wilaya,
mkoa na kanda.
Alisema mameneja hao watapimwa kwa kutumia
vigezo vitatu ambavyo ni kuongeza makusanyo ya
mapato, kuongeza idadi ya wateja wapya
waliounganishwa na huduma ya umeme na
ubunifu wa kutatua matatizo ya umeme katika
maeneo wanayoyasimamia.
“Mfano unakuta nguzo za umeme zinaoza hadi
zinaanguka chini na hakuna hatua yoyote
inayochukuliwa wakati kuna meneja katika eneo
hilo la kazi, hii haikubaliki,” alisema Profesa
Muhongo.
Muhongo alisisitiza kuwa changamoto zilizopo za
upatikanaji wa umeme wa uhakika na usambazaji
wa nishati hiyo zisimamiwe kwa umakini ili ziweze
kutatuliwa ndani ya miaka mitatu.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe alisema
bado kuna jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa
umeme unawafikia wananchi wengi, hivyo alihimiza
Tanesco kufanya kazi kwa ufanisi ili izalishe
umeme mwingi na kusambaza kwa wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Dk Alex
Kyaruzi, alisema bodi hiyo ina uwezo wa kufanyia
kazi maagizo yaliyotolewa na Profesa Muhongo na
kuahidi kuwa watayatekeleza na kusimamia kwa
umakini Menejimenti ili ifanye kazi kwa ufanisi unaotakiwa.
HabariLeo
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.