0
Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Kenya amejitia kitanzi baada ya kupoteza dau la
shilingi 80,000 sawa na dola $800 aliloweka katika mechi za Euro 2016.
Kwa mujibu wa gazeti la Kenya la Daily Nation
mwanafunzi huyo alikuwa ameweka dau la dola $ 400 kwa ushindi wa Ujerumani na pesa zingine
sawa na hizo kwa ushindi wa Italia.
Hata hivyo kinyume na matarajio yake mechi hiyo iliishia sare na kumaanisha kuwa alikuwa amepoteza pesa hizo zote.
Alifunga safari kutoka mjini Nairobi hadi kwao
magharibi mwa Kenya alipojitia kitanzi nyuma ya nyumba ya mamake mzazi katika kijiji cha Ondome Uriri jimbo la Nyanza.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo David Kirui anasema kuwa marehemu aliacha ujumbe akisema
hakuona haja ya kuendelea kuishi baada ya kupoteza pesa alizopewa za kulipia karo za chuo kikuu.
Ujerumani hata hivyo ilishinda kwa mikwaju ya penalti ilyofuatia.
Ujerumani itachuana dhidi ya wenyeji Ufaransa
katika nusu fainali baadaye leo.
Mshindi kati yao atachuana dhidi ya Ureno iliyoizaba Wales mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa jana.
Sasa mipango ya mazishi imeanza huku swala la kuenea kwa michezo ya bahati na sibu ikizua tena mjadala miongoni mwa wapenzi wa kandanda na
jamii kwa jumla.


BBC

Chapisha Maoni

 
Top