0
Uingereza itakuwa na Waziri Mkuu mwanamke, ambaye atachukua majukumu kufikia mwezi
Oktoba.
Hii ni baada ya wabunge wa chama tawala cha Conservative kuwateua wagombea wawili waliokuwa wanaongoza kukabiliana kuamua nani
atakuwa kiongozi mpya.

Waziri wa mambo ya ndani Theresa May, ndiye anayepigiwa upatu sana kumrithi David Cameron kama kiongozi wa chama na waziri mkuu.
Waziri wa kawi Andrea Leadsom, ndiye mwanamke huyo mwingine.
Waziri wa Haki Michael Gove, aliyekuwa mmoja wa waliopigia debe Uingereza kujitoa Muungano wa
Ulaya, alimaliza wa tatu kwenye kura ya
akaondolewa.
Matokeo kamili yanatarajiwa mwezi Septemba.
Kinyang’anyiro cha sasa cha kuchagua kiongozi
mpya kilianza baada ya Bw Cameron kuamua
kung’atuka.
Hii ni baada ya upande wake, uliotaka Uingereza
isalie EU, kushindwa kwenye kura ya maoni mwezi
uliopita.

Chapisha Maoni

 
Top