0
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema serikali yake itaendelea na mpango wa
kuwahamishia Wayahudi wa Ethiopia hadi nchini Israel.

Amesema serikali yake itahakikisha Wayahudi waliokwama nchini Ethiopia wanasafiri kujiunga na jamaa zao ambao tayari wamefika Israel.
Takriban Waethiopia 9,000 wanaodai kuwa
Wayahudi wanasubiri kuhamia Israel, na
wamesubiri kwa miaka mingi.
Akihutubia wanahabari mjini Addis Ababa, bw Netanyahu amesema shughuli hiyo itatekelezwa
hivi karibuni ingawa hakueleza ni wakati gani.
“Kuhusu kuwapeleka Israel watu wa jamii (Wayahudi Waethiopia) ambao bado wapo hapa,
tunafanya hivyo, tuliahidi, na tutatimiza ahadi hiyo kwa ngazi ya utu kuhakikisha familia zinaungana tena,” amesema.
“Haitafanyika siku za baadaye, bali itafanyika sasa
chini ya bajeti ya sasa. Tumejitolea katika mpango Fulani na tutaukamilisha.”.
Takriban Wayahudi Waethiopia 130,000 wanaishi Israel kwa sasa, tangu shughuli ya kuwahamisha
ianze 1984.
Serikali ya Israel hata hivyo imeshutumiwa kwa
kutohakikisha Wayahudi Waethiopia wanaingiana vyema na kukubalika katika jamii Ethiopia.
Miezi ya karibuni, mamia ya Wayahudi Waethiopia wameandamana Israel wakidai kubaguliwa.



BBC

Chapisha Maoni

 
Top