Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro
amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na
masuala ya soka.
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), imetangaza kumfungia
Muro kupitia ile kesi yake kwamba
amekuwa akiipinga na kuishambulia TFF
kwenye vyombo vya habari.
Kikao cha Kamati ya Maadili ya TFF, kilikaa
leo bila ya Muro kuwepo kwa kuwa wakati
mwaliko unatoka alikuwa nje ya Dar es
Salaam.
Katika makosa matatu aliyoshitakiwa, moja
amekumbana na adhabu hiyo, moja
amepigwa faini ya Sh milioni 3 na moja
ameonekana hana hatia.
Awali Muro alisema alikuwa mapumzikoni
Machame mkoani Kilimanjaro ambako ni kwao.
Chapisha Maoni