Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam wiki moja na nusu iliyopita
timu hizo zilitoka sare ya 1-1
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya
Kombe la Shirikisho Afrika CAF,hatua ya makundi
Yanga leo watakuwa na kibarua kigumu wakati
watakapo ikabili Medeama SC ya Ghana pambano
likipigwa uwanja wa Sekondi Takoradi nje kidogo
ya mji mkuu wa Accra.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 12 za jioni
kwa saa za Tanzania ambapo Ghana itakuwa saa
10 : jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani
mkali kutokana na ubora wa timu zote mbili.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam wiki moja na nusu iliyopita
timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 1-1
wenyeji Yanga wakitangulia kufunga mapema
dakika ya pili lakini Medeama wakasawazisha
dakika ya 17 na kufanya timu hizo kuendelea
kubaki kwenye nafasi za tatu na nne.
Yanga watahitaji ushindi katika mchezo wa leo
ili waweze kujinasua mkiani mwa kundi hilo na
kufufua matumaini ya kucheza nusu fainali
endapo watashinda mechi zao mbili zitakazo
salia huku wakiwaombea mabaya wapinzani wao
MO Bejai ya Algeria na Madeama zipate matokeo
mabaya kwenye mechi zao zijazo.
Kocha Hans Pluijm kitamkosa beki Vicent
Bossou, kutokana na kuwa na kadi mbili za njano
lakini nafasi yake huenda akachukuliwa na
nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye hiyo
itakuwa mechi yake ya kwanza tangu kuanza kwa
hatua hiyo ya makundi.
Pamoja na kuzidiwa na wapinzani wao Medeama
katika mchezo wa kwanza, Pluijm, ameondoka
nchini akiwa na matumaini makubwa ya kupata
ushindi katika mchezo huo wa kesho huku
akiwatumaini washambuliaji wake wawili Donald
Ngoma na Obrey Chirwa ambao wameonekana
tishio kwa wenyeji wao.
Pluijm alisema ameupa uzito mkubwa mchezo
wa leo kwasababu ndiyo uliobeba matumaini
yao ya kufika kule ambapo walipakusudia wakati
wanajiandaa na hatua hiyo ya makundi na hiyo
inatokana na maandalizi ambayo wameyafanya
kabla ya kuondoka nchini.
“Tutawakosa Bossou na Deusi Kaseke, lakini
waliobaki wote wapo katika hali nzuri na
ninafurahi kuona wachezaji wangu wote katika
hali nzuri kuelekea mchezo huo naamini
tutawashangaza wenyeji wetu Medeama kwa
kuwafunga wakiwa nyumbani kwao,”amesema
Pluijm.
Kocha huyo alisema kwakua wanahitaji pointi tatu
katika mchezo huo hawatocheza kwa kujihami
bali watacheza kwa kushambulia zaidi huku
akijaza viungo wengi katikati ili kusaidia ulinzi
kwasababu wapinzani wao wanatumia sana
mashambulizi ya kustukiza.
Kwaupande wao Medeam ambao wanashika
nafasi ya tatu kwenye kundi hilo wakiwa na pointi
mbili, wametamba kuimaliza Yanga katika
mchezo huo kwasababu wanawajua vizuri
wapinzani wao baada ya kuwaona katika mchezo
wa kwanza ulioisha kwa sare ya 1-1.
Kocha Pride Yaw Owusu, alisema Yanga ni timu
ngumu na nzuri lakini amewaanda vyema vijana
wake kuhakikisha wanapambana kwa dakika zote
90, ili kupata ushindi ambao utawahakikishia
kucheza hatua inayofuata ya nusu fainali.
“Najua kama Yanga wamekuja na nguvu kubwa
ya kutafuta ushindi wakiwa ugenini lakini hata
sisi tunahitaji pointi tatu ambazo zitatuweka
kwenye nafasi nzuri ya kumaliza wapili kwenye
kundi letu ili tucheze nusu fainali hivyo hatuta
kubali kupoteza mchezo huo hata kidogo,”
amesema.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni