Pluijm anafikiria kukifanyia marekebisho kikosi
chake kwa kutaka kuongeza wachezaji wapya
kwa lengo la kukiimarisha kikosi hicho kabla ya
msimu mpya wa Ligi Kuu
Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm, anafikiria
kukifanyia marekebisho kikosi chake kwa kutaka
kuongeza wachezaji wapya kwa lengo la
kukiimarisha kikosi hicho kabla ya msimu mpya
wa Ligi ya Vodacom kuanza Agosti 20.
Pluijm ameiambia Goal, sababu ya kufanya hivyo
ni kutokana na matokeo mabaya yasiyo ya
kuridhisha ambayo yameiweka timu hiyo katika
wakati mgumu kufuzu hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo mikubwa Afrika.
“Tatizo letu kubwa ni kiungo namba sita ambaye
kiuhalisia hawezi kupatikana Tanzania kwa
sababu wachezaji wengi wa Tanzania hawana
nguvu na hawajui kuimudu vyema nafasi
hiyo,”amesema Pluijm.
Yanga inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi
A, la michuano hiyo ya Afrika baada ya
kujikusanyia pointi moja katika michezo minne
iliyocheza na hivyo kupoteza matumaini ya
kuiona timu hiyo ikicheza nusu fainali.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni