Kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool ya Uingereza, Brendan Rodgers, amekataa kuifundisha timu ya nchi hiyo na amedai kwamba ndoto zakekwa sasa ni kuifundisha klabu ya Celtic ya nchini Scotland.
Kocha Roy Hodgson, ameamua kuachana na timu
hiyo ya taifa ya England mara baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini
Ufaransa, hivyo baadhi ya makocha ambao wametajwa kuchukua nafasi ya Hodgson ni
Rodgers.
Hata hivyo, Rodgers tayari amesaini mkataba wa kuifundisha klabu ya Celtic na amesema hawezi
kuachana na klabu hiyo kwa ajili ya England.
“Nilikuwa shabiki wa Celtic kwa muda mrefu na sasa nimekuwa kocha wa timu hii, ni ndoto
kwangu ya muda mrefu lakini sasa imekamilika na
ninafuraha kubwa kuwa kocha wa timu hii ambayo ina mashabiki wengi.
“England ni timu kubwa duniani na ina wachezaji
wenye uwezo mkubwa na majina makubwa, lakini
sina mpango wa kuwa kocha wa timu hiyo
ninaamini ni timu ngumu kwa mimi kuifundisha.
“Nimeshangaa kuona kocha Hodgson kuachana na
timu hiyo, ninaamini ana uwezo mkubwa sana,
hivyo siwezi kufanya makubwa kama ambavyo
yeye amefanya japokuwa kuna watu wanaamini
naweza kufanya hivyo,” alisema Rodgers.
Hata hivyo, tayari timu hiyo ya England
imefanikiwa kupata kocha wa muda, Gareth
Southgate, ambaye atakuwa ndani ya timu hiyo
hadi pale kocha mpya atakapopatikana.
Chapisha Maoni