kupelekea kujitoa kwenye kolabo aliyoshirikiswa na
TID kwenye wimbo wa Confidence, televisheni ya
EATV ilifanya mahojiano na msanii huyo.
Kwanza aliulizwa anajisikiaje kufanya kazi na TID
na suala la Dully kujitoa kwenye ngoma ya
Confidence analichukuliaje hilo? Joj Makini alisema
yeye yupo ok na hana tatizo kabisa na Dully hivyo
hakuona tatizo lolote la yeye kuingiza mistari yake
katika goma hiyo ya TID.
Joh pia ameweka wazi juu ya mipango yao
ambayo wamekuwa wakiiongea mara kwa mara na
Dully ya kufanya wimbo wa pamoja lakini
haijatokea tu nafasi na muda wa kufanya kazi ya
pamoja na mashabiki wategemee kolabo la yao
siku zijazo.
Pamoja na mambo mengine Joh anategemea
kuachia video ya ngoma yake mpya hivi karibuni
na kusema ndani ya miezi mitatu ijayo mbeleni
atatoa ngoma mpya na huwa anachelewa kutoa
ngoma kwani anaamini mziki wake unadumu sana.

Chapisha Maoni