amefungukia ugomvi ambao hutokea mara
kwa mara na shosti wake ambaye pia ni
muigizaji, Aunt Ezekiel usiingiliwe na mtu
kwani wanapogombana tofauti zao
wanazimaliza wenyewe na si mtu mwingine
yeyote.
Akizungumza na Amani Wema alisema kuwa,
yeye na Aunt ni watu waliopo karibu sana na
wanaopendana hivyo inapotokea
wanagombana huwa ni kitu kidogo kwao kwani
huyamaliza na maisha yanaendelea kama
kawaida.
“Jamani nyinyi mtuache tu, tunatibuana na
Aunt, tunajuana vizuri sana ugomvi wetu ni wa
mara kwa mara lakini tunamalizana wenyewe
kwa sababu ukweli ni kwamba hatuwezi kukaa
mbalimbali kwa muda mrefu kutokana na
kupendana,” alisema Wema.
Chanzo:GPL
Chapisha Maoni